Image
Image

Kiafya kama ulikuwa hujui nikwamba tangawizi ni tiba ya mfumo wa ummeng’enyaji wa chakula.


Tangawizi ni moja ya kiungo ambacho husaidia sana kuleta ladha na harufu nzuri kwenye chai.
Miongoni mwa faida za kutumia tangawizi ni pamoja na kusaidia mfumo wa ummeng’enyaji wa chakula tumboni.
Tangawizi pia husaidia sana kwa wale wenye matatizo ya kuhisi maumivu mara kwa mara kwenye viungo, hivyo matumizi ya chai yenye tangawizi huwa na nafasi kubwa ya kutoa ahueni kwa wenye tatizo hilo.
Pia tangawizi husaida sana kwa wale wenye kusumbuliwa na mafua, unapotumia chai yenye tangawizi husaidia sana katika kutibu tatizo hilo.
Kwa wale kinamama ambao husumbuliwa na kichefuchefu wakati wa kipindi cha ujauzito, tangawizi ina nafasi kubwa ya kuondosha hali ya kichefuchefu, hivyo si lazima kutumia ndimu katika kuondosha hali hiyo.
Pamoja na hayo tangawizi pia hutumika kwa kutuliza maumivu ya tumbo yanayochangiwa na matatizo ya usagaji wa chakula, halikadhalika tangawizi husaidia sana kuongeza hamu ya kula.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment