LICHA
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuruhusu idadi ya
wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na Klabu za Ligi Kuu kuwa saba
badala ya tano, shirikisho hilo limetoa masharti kwa klabu hizo kuingia
mikataba na wachezaji inaowahitaji.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Baraka
Kizuguto,mchezaji atakayesajiliwa awe ni wa timu za taifa za nchi yake
(wakubwa, U23, U20, U19 na U17 n.k.), awe anacheza katika Ligi Kuu ya
nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.
Kizuguto alisema kila
mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa
vijana ya dola 2,000 kwa kila msimu atakayocheza hapa nchini. Fedha hizi
zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira (Football Development
Fund).
"Pia imeamriwa kuwa mikataba ya klabu na wachezaji iliyo hai
itaendelea kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini
wataruhusiwa kuongeza mikataba yao iwapo watakubaliana na klabu zao,"
alisema.
Alisema kuanzia sasa mikataba kati ya wachezaji na klabu
itakayotambuliwa na TFF, itakuwa ni ile ambayo ni nakala halisi
zilizopigwa mhuri na lakiri ya TFF na kusajiliwa kwenye kumbukumbu ya
shirikisho hilo. Klabu na mwachezaji watapewa nakala hizi baada ya
kusajiliwa na TFF.
LESENI ZA MAKOCHA
Kamati ya utendaji imeamua
kuwa kuanzia msimu huu, Kocha wa timu ya ligi Kuu sharti awe na leseni B
ya CAF au itakayolingana nayo kutoka katika mashirikisho mengine
duniani na kocha msaidizi awe na leseni C ya CAF, hii ni kwa misimu
mitatu.
Kuanzia msimu wa 2018/19 kocha wa Ligi Kuu atatakiwa kuwa na
leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo kutoka katika mashirikisho
mengine duniani.
Aidha, Kamati ya Utendajji ya TFF imemteua Meshack
Bandawe kuwa mjumbe wa bodi ya mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu -
TFF (FDF), Bandawe ni meneja wa PPF Kanda ya Ziwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment