Kenya imetangaza vita kwa
walanguzi wanaofadhili wapiganaji wa Somalia ikiwa pamoja na kuwaandikisha na kuwapatia wasajiliwa mafunzo
ya kijeshi.
Chini ya hatua hiyo mashirika ya
usalama na washirika wao pia wata angalia wapiganaji wa kigeni wa Jihadi ambao wimbi lao limelaumiwa kuhusika
na mashambulio yanayozidi kuongezeka nchini Kenya.
Wakati majeshi ya Kenya
yanakwenda Somalia mwaka 2011 taarifa
zilionyesha kundi la al-Shabaab
lilikuwa na wapiganaji 400 kutoka nje wakiwemo wa nchi za magharib i
lakini idadi hiyo imeongezeka kwa kasi
hasa mwaka uliopita.
Kupambana na wafadhili wa
al-Shabaab ni sehemu ya mkakati mpya
uliotangazwa serikali ya Kenya
mara baada ya mashambulio kwenye Chuo Kikuu cha Garisa karibu na mpaka
wa Somalia Aprili mwaka huu ambapo watu 148 wengi wao wanafunzi
waliuawa.
0 comments:
Post a Comment