Zanzibar. Ushindi wa Uganda wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania juzi kwenye Uwanja wa Amaan uilikuwa ni mazishi rasmi ya kibarua cha kocha Mart Nooij kuendelea kuinoa Taifa Stars.
Kibarua cha Mdachi huyo kilionekana tayari kimekufa tangu Stars alipofungwa michezo mitatu kwenye mashindano ya Cosafa yailiyofanyika Afrika Kusini na wadau wakitaka kocha huyo atimuliwe.
Kutokana na matokeo hayo Kamati ya Utendaji ilikutana na kufikia uamuzi wa kumpa kocha huyo jukumu kuhakikisha anaifunga Uganda ili timu hiyo ifuzu kwa kucheza Fkwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (ChanHAN han2016, Rwanda).
Kipigo cha mabao 3-0 kimeiweka Taifa Stars katika wakati magumu wa kushinda mchezo wa marudiano utakaofanyika Uganda, ndipo kamati ya utendaji wa TFF ilipoamua kusitisha mkataba wa kKocha Nooij saa 5 usiku juzi Jumamosi kwa mtindo wa aina yake ambayo pengine hata yeye mwenyewe hakuuitegemea.
Minong’ono kuwa safari ya Nooij imefikia kikomo ilianza kusikika kwenye Uwanja wa Amaan mara baada ya Uganda kutangulia kupata bao la kuongoza kipindi cha kwanza ambapo viongozi wa TFF walionekana kukaa vikundi vikundi jukwaani wakijadili jambo.
Mara baada ya mechi kwisha, Nooij alkizungumza na wanahabari kwa dharau kwa kuwa bado alikuwa ana uhakika na kibarua chake licha ya kipigo hicho kwani yeye aliajiriwa na TFF na mkataba wake bado haujamalizika.
“Suala la kutimuliwa silitambuia na wala sina mpango wa kujiuzulu kwa sasa kwa sababu kuna kazi hapa bado sijaimaliza ndani ya hii timu. Nina mkataba na TFF na sio waandishi wa habari au hao mashabiki ambao wanapiga kelele,” alisema Nooij.
Wakati Nooij anatoa kauli hiyo, viongozi wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambao wote walikuwaepo visiwani Zanzibar walikaa kikao cha dharurra chini ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi ambacho kilidumu kwa zaidi ya saa moja na nusu.
Wakati huo kundi kubwa la mashabiki wa soka waliooonyeshwa kuchukizwa na matokeo ya kufungwa na Uganda walikuwa wamekaa nje ya Uwanja wa Amaan kusubiria nini ambacho kitaamuliwa na kikao hicho cha dharura.
Baada ya wajumbe kumaliza kikao hicho, Malinzi pamoja na Katibu wake CSelestine Mwesigwa walibaki peke yao kujadiliana jambo, naambapo rais huyo alionekana akimuhimiza kitu Mwesigwa.
Hata hivyo Malinzi alipotoka aligoma kuzungumza na wanahabari kuhusu kile kilichojadiliwaamuliwa na kikao hicho akiwataka kuwa na subira kwani maelekezo yote amempa katibu na Watanzania watafurahi ndani ya kipindi cha dakika thelathini zijazo.
Dakika kumi baadaye TFF kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura ilitoa taarifa kuwa mkataba wa Kocha Nooij umesitishwa sambamba na kuvunja benchi lote la ufundi, huku shirikisho likiahidi kutangaza benchi jipya la ufundi ndani ya siku chache zijazo.
0 comments:
Post a Comment