Mwimbaji anayedaiwa kuelekezewa maneno hayo ni
mkongwe wa siku nyingi, Khadija Kopa ambaye alishadai kwamba aliwahi kuonyesha
njia ya kutaka kushirikiana na mwenzake huyo lakini ameonekana kumkwepa bila
sababu za msingi.
Wakati Mzee Yusuph akijitapa jukwaani, Khadija Kopa
alidai alimtafuta mara kadhaa ili waimbe wimbo wa kushirikiana kama mfalme na
Malkia lakini mwenzake huyo amekuwa akimkwepa ishara inayoonyesha kwamba hataki
kushirikiana naye ingawa hajui sababu za hilo.
“Mimi nilishamfuata Mzee Yusuph nikitaka
tushirikiane tutoe wimbo kama yeye Mfalme nami Malkia, lakini mwenzangu naona
kama hapendi maana amekuwa akinikwepa na wimbo tulioshirikiana ni kwa sababu ya
shirika moja wapo lilitukutanisha kila mtu kwa wakati wake tukafanya kazi kwa
kuwa ni ya shirika na ilikuwa inalipa, lakini kwa wimbo wetu amekuwa akinikwepa
na sijui sababu zake,” alieleza Khadija Kopa.
Baadhi ya maneno aliyojinadi nayo Mzee Yusuph usiku
wa juzi katika ukumbi wa Mlimani City, ni pamoja na kutaja baadhi ya majina ya
wasanii walipo katika muziki huo na kutomtaja Malkia wa muziki huo, Khadija
Kopa, huku akidai hawajui wasanii wengine jambo lililozua minong’ono kwa
wahudhuriaji wa tuzo hizo. Katika tuzo hizo, Mzee Yusuph alinyakua tuzo tatu
ikiwemo msanii bora wa kiume wa taarabu, mtunzi bora wa mwaka wa taarabu pamoja
na kikundi bora cha taarabu cha Jahazi Modern Taarabu.
0 comments:
Post a Comment