Naibu
katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Zanzibar SALUM MWALIM amefanya
ziara ya kutembelea vituo vya kujiandikishia wapiga kura katika wilaya za
ilemela na nyamagana mkoani Mwanza na kushuhudia kasi ndogo ya uandikishaji na
uchache wa mashine za kielektroniki
zisizoendana na idadi kubwa ya wananchi wanaojitokeza kujiandikisha.
Kufuatia hali
hiyo,naibu katibu mkuu wa chadema Zanzibar SALUM MWALIM ameonyesha wasiwasi wa
kutofanikiwa kwa zoezi hilo katika baadhi ya vituo alivyovitembelea kutokana na
wananchi kutumia zaidi ya siku tatu vituoni bila kuandikishwa na kusababisha
baadhi yao kuanza kukata tamaa, huku mizengwe, upendeleo na vitendo vya rushwa
vikidaiwa kutawala zozi hilo lililoanza juni 9 mwaka huu katika baadhi ya kata
za wilaya ya ilemela na nyamagana.
Baada ya naibu
katibu mkuu huyo kusikiliza kilio cha wakazi wa mkoa wa Mwanza ambao
wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kujiandikishia ili
kuhakikisha wanapata haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaowataka
katika uchaguzi mkuu ujao, nini ushauri wa naibu katibumkuu wa chadema Zanzibar
kwa watendaji wa tume ya taifa ya uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment