Akina mama hao wamefika mjini meatu majira ya saa mbili asubuhi
wakiwa ndani ya maroli na walipofika eneo la mjini mwanhuzi makao makuu ya mji
wa MEATU waliteremka na baada ya muda mkuu wa wilaya hiyo ERASTO
SIMA akiongozana na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo aliowaomba
warudi katika kijiji cha bukundi kwenye makao makuu ya kata hiyo ili aweze
kuongea nao lakini waligoma kata kata kurudi huko.
Baada ya viongozi wa akina mama hao kuwasihi ndipo walipokubalina
kwenda kwenye uwanja wa shule ya msingi,mwanuhzi ambapo waliandamana chini ya
ulinzi wa polisi na walipofika hapo walianza kutoa kilio chao cha kutaka wapewe
miili ya watoto wao na kwamba iwapo mkuu wa wilaya hatawasikiliza basi wataenda
kumuona rais kwani wamechoka na manyanyaso ya mwekezaji huyo.
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji nchini,GEORGE BAJUTA ambaye pia
alikuwepo katika mkutano huo amesema wafugaji hao wamekuwa wakiishi kama
wakimbizi katika nchi yao na kwamba sasa imetosha na hawataendelea kuvumilia
kuona wafugaji wakiuwawa kwa kupigwa risasi na mwekezaji huyo.
Akijibu malalamiko ya wafugaji hao mkuu wa wilaya hiyo amesema
serikali imelishughulikia kwa kina suala hilo ikiwa ni pamoja na kuwakamata
wahusika waliofanya tukio hilo ambapo pia bado wanaendelea na upelelezi wa
tukio hilo kauli ambayo hata hivyo akina mama hao waliipinga na kudai kuwa wa
serikali ya wilaya imekuwa haiwatendei haki bali imekuwa ikimtetea mwekezaji
kampuni ya mwiba.
Mbunge wa jimbo hilo meshaki opurukwa ameitupia lawama serikali
kwa madai kuwa suala hilo limekuwa la muda mrefu na mwekezaji huyo amekuwa
akiuwawa wafugaji na kutochukuliwa hatua ambapo alimtaka mkuu wa wilaya hiyo
kutangaza kuanzia leo kusikitishwa kwa shughuli za kampuni ya mwiba katika poli
hilo hadi muafaka wa miili ya watu hao ipatikane na pia ofisi ya mkuu wa wilaya
iwape chakula akina mama hao ambao wamegoma kurudi majumbani hadi wapate miili
hiyo kauri ambayo ilipingwa na mkuu wa wilaya hiyo kwa madai kuwa suala hilo
linashughulikiwa.
Hata hivyo hadi itv inatoka eneo la tukio hilo akina mama hao
walikuwa bado wamepiga kambi katika uwanja wa shule hiyo ambapo wamesema kamwe
hawataondoka na sasa wanajipanga kwenda kumuona rais ili kumueleza kilio chao .
0 comments:
Post a Comment