Ripoti hii ya pamoja iliyotolewa leo
imeangalia upatikanaji wa huduma zote za afya zikiwemo mpango wa uzazi, huduma
za wanawake wajawazito, chanjo kwa watoto, dawa za kupunguza makali ya ukimwi,
ARV, dawa za kutibu kifua kikuu na upatikanaji wa mafi safi na kujisafi kwa
mwaka 2013.
Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa,
Tessa Tan Torres Edejer, Mratibu wa Maswala ya mifumo ya afya wa WHO, ameeleza
kwamba sababu ya kwanza ya kukosa huduma za msingi ni umaskini.
" Hawapati huduma hizo kwa sababu hawana pesa ya kutosha kwa matibabu watakayopaswa kulipa, mfano dawa au chanjo. Pia inawezekana kwamba wanaishi mbali na vituo vya afya, na hawana pesa ya kwenda kituo cha afya. Sababu nyingine pia ni kwamba, hata kama vituo vya afya vipo, huenda havina dawa au wafanyakazi kuwahudumia."
Marie-Paule Kieny, Msaidizi wa Mkurugenzi
Mkuu wa WHO, amesema serikali zinapaswa kuwapatia huduma za afya watu maskini
zaidi, wanawake na watoto, wale wanaoishi mbali na wale kutoka vikundi vya
walio wachache.
WHO na Benki ya Dunia zinapendekeza kuwa
serikali zinazotaka kutekeleza huduma za afya kwa wote zilenge angalau asilimia
80 ya watu huku hata hivyo yakifurahia kuweza kupima mafanikio katika swala
hilo kwa mara ya kwanza, yakisema ripoti zingine kama hii zitatolewa kila
mwaka, ili kutathmini mafanikio ya nchi katika kufikisha huduma za afya kwa
wote
0 comments:
Post a Comment