Akizungumza baada ya kutembelea
ujenzi wa magorofa matatu ambayo yamejengwa na shirika hilo katika Manispaa
ya Mtwara- Mikindani amesema watu
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuishi Mtwara na kufanya
kazi katika sekta ya gesi na viwanda,hivyo ujenzi wa makazi hayo ni muhimu .
Waziri LUKUVI amesisitiza
kuwa lengo la serikali ni kuufanya Mkoa
wa Mtwara kuwa eneo la viwanda.
kwa upande wake Meneja wa
Shirika la Nyumba la taifa Mkoa wa Mtwara,JOSEPH JOHN amesema mikakati
ya shirika hilo ni kuendelea kujenga nyumba kama hizo,lakini tatizo linalikabili shirika kwa sasa ni gharama kubwa ya ununuzi wa vifaa
vya ujenzi.
0 comments:
Post a Comment