Naibu Waziri wa Maji,AMOSI MAKALA AMETOA KAULI HIYO Bungeni alipokuwa a kijibu swali la Mbunge wa Viti
Maalum , MARIA HEWA aloyeuliza ni lini
wananchi wataruhusiwa kunywa maji ya bomba moja kwa moja bila kuchemshwa.
Naibu Waziri wa Maji a mesema serikali itaendelea na
jitihada za upatikanaji wa majisafi na salama kwa kufanya maboresho ya mitambo
ya maji na ujenzi wa miradi mipya mijini na vijijini.
Katika hatua nyinine Serikali katika mwaka 2015 itaanza kutoa
mafunzo ya uandaaji wa minofu ya samaki kwa utaratibu wa kozi fupi ili
kuwawezesha walengwa kuendana na soko la ajira.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dakta. SHUKURU KAWAMBWA amesema hayo alipokuwa a kijibu swali la
mbunge wa Lindi Mjini, SALUM BARWANY
aliyeuliza serikali ina mpango gani wa kuwa na kiwanda cha minofu ya
samaki pamoja na ujenzi wa hoteli ili kutoa mafunzo kwa vijana.
Dakta. KAWAMBWA amesema serikali
imefikia hatua ya kutenga eneo la Mitwelo lenye ukubwa wa Ekari 32.5 ambapo
VETA imeshalipa gharama za fidia kwa manispaa ya Lindi.
0 comments:
Post a Comment