Lukuvi amesema kutokana na hali hiyo kuanzia sasa
kila mwananchi mwenye kiwanja au nyumba yake atalazimika kuuza kiwanja chake
kwa bei anayoitaka au kujenga nyumba kwa mujibu wa ramani ya mji mpya
Akizungumza na wananchi hao juzi katika mkutano
uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni
Dar es Salaam, Lukuvi, alisema sintofahamu iliyokuwapo ilitokana na hapo awali
wananchi kutowekwa wazi kuhusu mchakato wa uuzaji wa maeneo yao.
“Wananchi wamekuwa katika sintofahamu juu ya uuzaji
wa maeneo yao, wengine mnafikiri Serikali ndiyo itakayonunua ardhi yenu na
wengine mnafikiri ardhi inadalaliwa na Wakala wa Kusimamia Uendelezaji wa Mji
Mpya wa Kigamboni (KDA),” alisema Lukuvi na kuongeza;
“Hakuna Serikali itakayouza ardhi wala KDA kudalalia
ardhi yenu…wananchi wa Kigamboni ndiyo mtakaoamua juu ya uuzaji wa ardhi yenu
na serikali itakuwa mwangalizi ili wananchi wasiibiwe kwa kuuza bei ya chini
sana,” alisema Lukuvi huku umati huo ukimshangilia.
Alisema wananchi wanachotakiwa ni kuchagua mambo
matatu katika mpango huo ambayo ni kuuza ardhi yao wenyewe moja kwa moja kwa
wawekezaji, kuingia ubia na wawekezaji na kutafuta fedha za kujenga wenyewe.
Alisema kama mwananchi ataamua kujenga mwenyewe
atatakiwa kufuata ramani na mpango wa mji mpya unavyoonyesha.
“Mtu anaweza kuamua kujenga mwenyewe lakini si
kwamba unaamua kujenga unachotaka bali utajenga kilichopo kwenye mpango,
haiwezekani eneo la kujenga majengo makubwa ya biashara wewe ujenge choo,”
alisema Lukuvi.
Alisema ili kuhakikisha wananchi wanatekeleza mambo
hayo matatu ni lazima wapatiwe hatimiliki za maeneo yao suala ambalo awali
halikuwapo kwa madai kuwa hakuna haja ya kutoa hati kwa eneo ambalo tayari lipo
kwenye mpango.
“Katika suala la kutoa hati nilipingana na watu wa
Mipango Miji na nikawaambia lazima wananchi wapewe hati zao ili wakati wa
kufanya makubaliano na wawekezaji wawe na ushahidi wa kumiliki ardhi hiyo,”
alisema Lukuvi.
0 comments:
Post a Comment