KAMATI
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemwagiza
Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi kuunda Kamati Maalumu ya
kusimamia mchakato wa utoaji wa tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari
wa TFF, Baraka Kizuguto, hatua hiyo imekuja baada ya kuzingatia
upungufu uliojitokeza katika uteuzi wa tuzo za ligi hiyo msimu wa
2014/15.
"Kamati hii itazingatia umuhimu wa kuhusisha Idara za Ufundi
za TFF katika zoezi hilo na wadhamini na ligi watahusishwa kwa ukaribu
katika zoezi hili," alisema Kizuguto.
Kizuguto alisema katika kikao hicho kamati hiyo pia ilipitia rasimu ya kanuni za Ligi Kuu, FDL na SDL za msimu ujao wa 2015/16.
Alisema
mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kwenye maeneo yafuatayo: Kamati hiyo
imesisitiza kuwa hakuna klabu itakayopitishiwa usajili wake kama kupewa
leseni ya klabu ya msimu.
Kizuguto alisema kamati hiyo pia iliridhia
wazo la Kamati ya Maamuzi kuwa kuanzia msimu 2015/16 kutakuwa na jopo
maalumu ya waamuzi (Elite referees) litakalochezeshwa mechi zote za Ligi
Kuu.
"Waamuzi hawa watakuwa ni 16 wa kati, 32 wa pembeni na wanne wa akiba. Hii itasaidia kuongoza ufanisi katika uamuzi," alisema.
Katika
hatua nyingine,Kizuguto alisema klabu zimeongezwa mgawanyo wa mapato ya
milangoni na sasa zitakuwa zinachukua asilimia 60 ya mapato ya
mlangoni, makato mengine ni asiliamia 18 VAT na asilimia 15 gharama za
uwanja.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment