MWENYEKITI wa Yanga,
Yusuf Manji amesema anajisikia faraja kuwaongoza wanachama na mashabiki
wa klabu hiyo, kwani imemfanya aishi maisha ya mani yeye na familia
yake. Kutokana na kitendo hicho Manji ameahidi kuiongoza klabu hiyo vyema hadi hapo itakapofika mwisho wake. Akizungumza
Dar es Salaam jana na viongozi wa matawi mbalimbali ya klabu hiyo,
Manji alisema anajisikia faraja kuwa na marafiki wengi kuliko maadui
hivyo ana imani hata atakapostaafu ataendelea kuishi maisha ya upendo na
amani. Alisema anapata thawabu kuwaongoza wanachama na mashabiki
wa Yanga, ambao hufurahia kila timu yao na hali hiyo imekuwa ikimpa
furaha katika maisha yake. Mwenyekiti huyo alisema amefanya mambo
mengi mazuri ndani ya Yanga, tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza
akiwa kijana mwenye umri wa miaka 33. "Kutokana na mambo mazuri
niliyoyafanya wazee wa Yanga, walinichagua kuwa Chifu wa kwanza katika
klabu hii jambo ambalo ninajivunia nikiwa kiongozi hadi nitakapostaafu
uongozi wangu," alisema Manji. Alisema anajivunia kuwa Mwenyekiti
wa klabu hiyo kongwe nchini akiwa na miaka 36 hadi sasa na kwamba
anashukuru kuona Yanga, mpaka leo inafanya vyema katika michuano
mbalimbali.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment