Image
Image

Mawaziri wajibu hoja kwa vijembe.



Karibu mawaziri wote waliosimama kutoa ufafanuzi wa sehemu zinazogusa wizara zao, walitumia nafasi hiyo kuwananga wapinzani, kujigamba kwa mafanikio ya Serikali na kutamba kuwa watarudi kwa wingi bungeni mwakani, hivyo kulitaka Bunge kuongeza viti mwaka huu.

Tambo,kejeli, vijembe na kampeni vilitawala bungeni mjini hapa jana wakati mawaziri wakijibu hoja za wabunge wa upinzani waliokosoa Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2015/16.
Karibu mawaziri wote waliosimama kutoa ufafanuzi wa sehemu zinazogusa wizara zao, walitumia nafasi hiyo kuwananga wapinzani, kujigamba kwa mafanikio ya Serikali na kutamba kuwa watarudi kwa wingi bungeni mwakani, hivyo kulitaka Bunge kuongeza viti mwaka huu.
Kutokana na mwaka huu kuwa mwisho kwa Serikali ya Awamu ya Nne, bajeti ilizungumzia mafanikio ambayo Serikali imeyapata kwa kipindi cha miaka mitano, lakini wapinzani waliikosoa wakisema imeshindwa kuwaondolea Watanzania umaskini, huku wakidai CCM imechoka na hivyo isipewe nafasi ya kuendelea kuongoza nchi.
Kauli hizo za wapinzani ziliwafanya mawaziri waliozungumza jana kutumia muda mwingi kuisifu Serikali ya CCM na kuwaponda wapinzani.
Aliyefungua dimba ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Henry Mwanry, ambaye alionyesha kuchukizwa na kauli za wapinzani kuwa Serikali haijafanya chochote.
“Inasikitisha kuwa hata kinachoonekana hakisemwi na kauli zinazotolewa ni kuwa ‘hawafai, ondokeni, tupeni nchi’ na sasa nasema, Serikali songa mbele kwa mbele,” alisema.
Mwanry alisema mwaka 2010 kulikuwa na hospitali 179 za wilaya, lakini sasa zipo 242, vituo vya afya vimeongezeka kutoka 620 hadi 723 na zahanati kutoka 5,400 hadi 6,034.
Alisema katika sekta ya elimu, mwaka 2010 shule za sekondari zilikuwa 3,397 sasa zipo 4,753. Walimu wameajiriwa kutoka 30,252 wa mwaka 2010 hadi 80,529 wakati maabara za sayansi zilikuwa 1,113 sasa zipo 5,979 na 4,237 ziko katika hatua mbalimbali.
“Tupeni moyo jamani, tumefanya kazi. Tusifieni basi, haiwezekani mafanikio yote haya halafu mnasema hakuna kitu,” alisema Mwanry akigeukia upande wanaokaa wabunge wa upinzani.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alianza kwa kupangua hoja iliyotikisa Bunge ya tozo ya mafuta kwa kusema kuwa hoja iliwasilishwa kishabiki.
Alisema kuwa Kambi ya Upinzani inadhani kuwa CCM inaweza kufanya mambo na kuwafanya watu waonekane kama wako peponi. “Hatuwezi kuleta pepo, tutafanya kwa utaratibu,” alisema. “Watu wanasema tozo ya mafuta, sasa wanataka wasione umeme majimboni mwao? Sasa mimi nasema hadi kufikia Juni 30 au Julai mwishoni, miradi ya umeme itakuwa imemalizika Hata maeneo ambayo umeme umepita, tumenunua transfoma 4,000.
“Kuhusu bomba la gesi, mradi umekamilika kwa asilimia 90, nirudisheni nimalizie haya tunayoyafanya, msiniache, msiniangushe.”


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment