KIKOSI cha timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam kimeendelea na mazoezi huku wachezaji wake wakiwa wameongezeka na kufikia 18.
Kwa sasa kikosi hicho kinaendelea na mazoezi huku kikimkosa mshambuliaji wake Simon Msuva pamoja na kiungo Haruna Niyonzima.
Awali
kikosi hicho kilianza mazoezi na wachezaji wachache kutokana na baadhi
yao kujiunga na timu ya Taifa, Taifa Stars huku wachezaji wao wakigeni
wakiwa bado wapo likizo.
Wachezaji wa kigeni wa timu hiyo Andrey
Coutinho pamoja na Kipha Shemarn walijiunga katika mazoezi na kikosi
chao wiki iliyopita wakitokea mapumzikoni.
Katika mazoezi hayo wachezaji walionesha umahiri mkubwa huku Lansana Kamara akiendelea kudhihirisha ubora wake.
Wachezaji wa yanga wakisali kabla ya kuanza mazoezi(Picha na Maktaba Yetu).
Akizungumza baada ya mazoezi hayo Kocha Mkuu wa wa timu hiyo, Mholanzi Hans van de Pluijm alisema kuwa kwa sasa nguvu zao zote wanazielekeza katika mchezo wao wa kirafiki wa Julai 27, mwaka huu dhidi ya Sports villa ya Uganda utakaochezwa uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.
Alisema kuwa mchezo huo utakuwa ni kipimo tosha kwa wachezaji wake na yeye kama mwalimu kuweza kujua ubora wa wachezaji wake.
"Hii itakuwa mechi ya kipimo kwetu pia tutaitumia kujua ni maeneo gani ambayo yana mapungufu ili tuweze kuyafanyanyia kazi mapema," alisema Pluijm.
Yanga imepania kuwa na kikosi tishio katika msimu ujao wa ligi kuu baada ya kuchukua ubingwa wakiwa na mechi mbili mkononi katika msimu uliopita.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment