ARGENTINA itamenyana na Colombia ya Radamel Falcao katika Robo Fainali ya Copa America Ijumaa hii nchini Chile.
Wenyeji Chile watamenyana na Uruguay katika Robo Fainali ya kwanza kwsho wakati keshokutwa Bolivia watamenyana na Peru.
Robo
Fainali ya mwisho itachezwa Jumamosi kati ya Brazil na Paraguay. Brazil
imetinga Robo Fainali kwa wa mabao 2-1 dhidi ya Venezuela usiku wa
kuamkia jana.
Ratiba kamili ya michuano hiyo ni Chile v Uruguay
(kesho) Bolivia v Peru (Alhamisi) Argentina v Colombia (Ijumaa) na
Brazil v Paraguay (Jumamosi).
Ikicheza bila ya nyota tegemeo lake,
Neymar aliyefungiwa mechi nne kwa utovu wa nidhamu aliouonesha katika
mchezo dhidi ya Colombia, Brazil ilipata mabao yake kupitia kwa Thiago
Silva dakika ya tisa na Roberto Firmino dakika ya 51.
Fedor ndiye mfungaji wa bao pekee la Venezuela, aliyemtungua kipa Jefferson zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika.
Colombia
imelazimishwa sare ya 0-0 na Peru, huku mshambuliaji Radamel Falcao
akitolewa uwanjani dakika ya 65 baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya
ukuta wa Peru.
Sare hiyo inazifanya timu zote hizo zimalize mechi za
Kundi C na pointi nne kila moja na Peru inakwenda Robo Fainali moja kwa
moja kama mshindi wa pili nyuma ya Brazil.
Sare hiyo pia inaitupa nje
ya michuano hiyo Ecuador iliyokuwa Kundi A,ambayo imemaliza na wastani
mbaya zaidi kati ya washindi wa tatu wa makundi yote.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment