Uamuzi wa wazazi hao kuingilia kati ni kile walichodai kuwa wameuvumilia mgogoro
huo kwa muda mrefu kwani ni zaidi ya miezi sita watoto wao hawajahudhuria
masomo hivyo hatua iliyobaki ni kwenda kuonana na rais wa jamhuri ya muungano
Dkt.Jakaya Kikwete ili kujua hatma ya hili.
Wakizungumza na Tambarare Halisi iliyotaka kujua
kuwa licha ya matangazo yanayo tolewa juu ya kurejea chuoni hapo je wao wana
msimamo gani? Wanafunzi wanao soma kozi ya famasia Walisema kuwa hawawezi
kurudi hadi kozi hiyo itakapopata usajili kwani kila mara wamekuwa wakiahidiwa
bila mafanikio huku wakiomba serikali kuwahamisha kama suala la usajili
limeshindikana.
Kufuatia sakata hili ambalo limeonekana kuchuua muda
Tambarare Halisi ilifika wizara ya afya na ustawi wa jamii ili kupata ufafanuzi juu ya
mgogoro huo lakini cha kustaajabisha msemaji wa wizara hiyo Nsachris Mwamaja
ambaye hakutaka kurekodiwa amedai wizara haihusiki na mgogoro huo na kwamba uko
mikononii mwa kamati iliyoundwa na bunge kwa ajili ya kulifuatilia.
Hivi karibuni Waziri waelimu na mafunzo ya ufundi
Dkt.Shukuru Kawambwa alipiga kambi chuoni hapo ilikuweka mambo sawa lakini
juhudi ziligonga mwamba na kudai waziri wa afya ndiye atakaye limaliza suala
hilo.
0 comments:
Post a Comment