Mazungumzo kati ya serikali na
vyama vya upinzani nchini Burundi yanatarajia kuanza tena leo katika juhudi za
hivi karibuni za kutatua mgogoro wa nchi hiyo.
Mazungumzo hayo yanakuja huku
wachambuzi wakisema kuanza kwa mazungumzo hayo mapya kunaweza kusaidia kuleta
muafaka wa matatizo yaliyogubika uwanja wa siasa wa nchi hiyo.
Burundi imekumbwa na machafuko ya
maandamano na jaribio la mapinduzi kupinga uamuzi wa Rais PIERRE NKURUNZIZA
kutaka kugombea muhula wa tatu.
Umoja wa Ulaya umeionya Burundi
kwamba huenda ukaiwekea vikwazo kwa wote wanaohusika na machafuko na kufikiria
hatua nyingine dhidi ya taifa hilo linalotegemea misaada.
Watu wapatao 70 wameripotiwa kufa
na maelfu ya wengine kukimbia makazi yao kutokana na machafuko yaliyoikumba
nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment