Hayo yamebainishwa na mtaalam wa
afya Dr.Ringo Ernest katika shule ya msingi Ungindoni iliyoko Kigamboni jijini
Dar es salaam wakati baadhi ya wahudumu wa afya walipoitembelea shule hiyo na
kufanya zoezi la kuwapatia huduma ya dawa za minyoo na kushiriki katika zoezi
la kufanya usafi shuleni hapo ambapo Dr.Ringo amedai kuwa minyoo kwa kiasi
kikubwa inachangia kwa watoto wanaokuwa hususani wale wa shule ya msingi kushindwa
kufanya vizuri katika mitihani yao na kuwahamasisha wazazi kuhakikisha watoto
wao wanapata dawa za minyoo kwa wakati.
Nao baadhi ya wanafunzi na walimu wamesema shule
hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa madarasa ya kutosha
pamoja na madawati na kutoa wito kwa watu wanaoipenda sekta ya elimu kusaidia
kukabiliana na changamoto hizo.
0 comments:
Post a Comment