Mkutano wa dharura wa Umoja wa
Ulaya uliofanyika Brussels,Ubelgiji umefanya viongozi wa umoja huo waonyeshe
matumaini ya kufikiwa muafaka wa kuepusha Ugiriki kushindwa kulipa madeni yake.
Katika mkutano huo Serikali ya Ugiriki
ilijitolea kuchangu YURO BILIONI nane
kwa kuongeza ushuru na kupunguza matumizi katika miaka miwili ijayo ili
kuwaridhisha wajosamo wake wanaoikopesha.
Kiongozi wa Ujerumani, ANGELA
MERKEL amesema mapendekezo yaliyotolewa yanaonyesha,lakini juhudi zaidi
zinahitajika na muda ni mfupi.
Ugiriki ni lazima ilipe kufikia mwishoni mwa mwezi huu YURO
milioni 1.6 inazodaiwa na Shirika la Kimataifa la -IMF.
0 comments:
Post a Comment