Image
Image

Mgombea urais ACT kujulikana Agosti 10.


Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba,  akiwahutubia wakazi wa mji wa Tabora juzi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya ,Town School, mara baada ya kuzindua Azimio la Tabora lililouhishwa kutoka azimio la Arusha.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Anna Mghira, akiwahutubia wakazi wa mji wa Tabora juzi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya ,Town School, mara baada ya kuzindua Azimio la Tabora lililouhishwa kutoka azimio la Arusha



Wakazi wa mji wa Tabora wakifuatilia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Town School, mara baada ya kuzindua Azimio la Tabora lililouhishwa kutoka azimio la Arusha.



Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwahutubia wakazi wa mji wa Tabora juzi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Town School, mara baada ya kuzindua Azimio la Tabora lililouhishwa kutoka azimio la Arusha.

Chama cha ACT - Wazalendo kinatarajia kumtagaza mgombea wake wa urais wa Agosti 10, imefahamika. Chama hicho kimesema mtia nia atakayepeperusha bendera ya ACT - Wazalendo atawajibika kutangaza mali binafsi na vyanzo vyake kwa kufuata utaratibu ulioanishwa katika katiba ya chama hicho.
Hayo yalisemwa jana mjini Geita na Kiongozi wa Chama hicho, Zitto Kabwe wakati akihutubia mamia ya wananchi katika viwanja vya Stand mjini hapa.
Alisema Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana juzi mjini Tabora, imepitisha ratiba kamili ya kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi mbalimbali za chama hicho kuanzia Julai Mosi.
“Kuanzia Julai Mosi mpaka Julai 17 ni kuchukua fomu kwa ngazi ya udiwani kwa ada ya Sh10,000, Julai 1-26 kuchukua fomu kwa ngazi ya ubunge na uwakilishi na ada yake ni Sh20,000 na kwa ngazi ya urais shughuli hiyo itakuwa kati ya Julai 1-26 na ada yake ni Sh100,000,” alisema Zitto na kuongeza:
“Vikao vya ngazi mbalimbali ya uteuzi vitaanza kuanzia Julai 27 hadi Agosti 10 mkutano mkuu wa chama utakapopitisha jina la mgombea urais.”
Sifa za mgombea urais
Zitto alisema lazima mgombea huyo awe amethibitika kuielewa itikadi, falsafa, misingi na sera za ACT - Wazalendo na aonyeshe utayari wa kuisimamia na kuiishi, awe ni mtu anayejitegemea kutokana na chanzo halali cha kipato kutokana na shughuli halali.
Alisema pia atakayetaka kukiwakilisha chama hicho kwa nafasi ya urais, itampasa kuwa mwenye haiba na taswira ya kuiwakilisha na kuipa heshima stahiki Tanzania katika Jumuiya za Kimataifa.
Chama hicho kinaendelea na ziara yake ya kulinadi azimio la Tabora lililozinduliwa juzi Mjini Tabora likilenga kuhuisha Azimio la Arusha. Leo watakuwa katika Mkoa wa Kagera.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment