Wananchi wa vijiji
18 vya Kata ya Kiria Wilayani
Mwanga Mkoani Kilimanjaro wanakabiliwa
na tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi hali inayowalazimu kunywa maji
ya bwawa la Nyumba ya Mungu ambayo ni hatari kwa usalama wa afya zao.
Wananchi hao wamesema
wanalazimika kunywa maji hayo kutokana na kukosekana kwa maji maeneo ya karibu na makazi ya wananchi hao wa ukanda wa
tambarare .
Wamesema tatizo hilo
linasababisha wakazi wa vijiji vya Kata hiyo kuugua magonjwa ya mlipuko kila
mwaka na kwamba wamekuwa wakipewa ahadi
za kuletewa maji kwa muda mrefu bila
mafanikio .
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiti cha
Mungu , Bwana EDIMUNDU MWAIPUNGU ame sema maji hayo ya bwawa hilo ni hatari
kwa afya za binadamu kutokana na bwawa hilo
kupokea maji machafu kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro
Mkurugeznzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mwanga , Bwana JAMUHURI WILI AM
anakiri kuwapo kwa tatizo hilo na kwamba kuna mradi unaotekelezwa kupeleka maji katik a kata hiyo ambao tayari
umesha anza na kwamba endapo utakamilika
utaondoa adha kwa wananchi wa vijiji 18 vya wilaya hiyo .
0 comments:
Post a Comment