Bwana Amano amesema hayo wakati kongamano la
kimataifa kuhusu teknolojia ya kompyuta katika ulimwengu wenye nishati ya
nyuklia, ambalo limeanza leo katika makao makuu ya IAEA mjini Vienna, Austria.
Amesema ingawa usalama wa nyuklia ni wajibu
wa kitaifa, IAEA ikiwa na nchi wanachama 164, ina wajibu muhimu katika kuusaidia
ulimwengu kuchukua hatua za pamoja dhidi ya tishio la ugaidi wa kutumia nishati
ya nyuklia.
"Magaidi na wahalifu wengine
hutekeleza vitendo vyao katika mitandao ya kimataifa, na wanaweza kushambulia
popote. Kwa hiyo kupambana nao ni lazima kuwe kwa kimataifa."
Hii ni mara ya kwanza kongamano kuhusu suala
la usalama wa kompyuta katika nyuklia linafanyika kwenye IAEA, likiwaleta
pamoja zaidi ya wataalam 650 kutoka nchi zinazozidi 100.
0 comments:
Post a Comment