Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq
amesema hayo wakati akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kufahamu
msimamo wa Umoja huko kuhusu hatua ya Burundi juu ya uchaguzi wa wabunge na
Rais.
Amesema Mjumbe maalum wa Umoja huo kwa maziwa
makuu Said Djinnit anaendelea na harakati za kukutana na pande zote
husika kwenye sintofahamu inayoendelea Burundi, sambamba na Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye..
Naamini anatarajia kuwasiliana baadaye
leo na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ili kupata habari kamili kuhusu hali
ilivyo sasa. Lakini hatimaye hili ni jambo ambalo linapaswa kuridhiwa na pande
zote. Hata hivyo tunahitaji kuhakikisha vyovyote watakavyokubaliana,
wataafikiana kuwa chaguzi zinazofanyika zinakuwa salama, halali na
jumuishi."
Alipoulizwa msimamo wa Umoja wa Mataifa
kufuatia kauli ya msemaji wa serikali ya Burundi kuwa suala la awamu ya tatu ni
la mamlaka ya nchi na si vinginevyo na hivyo hoja imefungwa, Bwana Haq amesema
Umoja wa Mataifa umekuwa unaeleza bayana kuwa makubaliano ya Arusha ni lazima
yazingatiwe na kwamba wananchi wa Burundi wenyewe wanaweza kukubaliana kuhusu
mustakhbali wao juu ya chaguzi huru, salama na haki.
0 comments:
Post a Comment