Akitangaza taarifa ya kifo hicho
leo Bungeni mjini Dodoma katiak bunge la bajeti linaloendelea naibu Spika Job Ndugai
amesmea marehemu mwaiposa alikuwa anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la Damua
ambalo ndilo limesababisha kifo chake
Kutokana na msibo huo Bunge la
bajeti limeahirishwa hadi alhamisi ambapo kesho mbunge huyo ataagwa mjini Dodoma
na kusafirishwa kuletwa jijini Dar es Salaam kwa mipango mingine ya mazishi.
Kwa upande wa Baadhi ya wabunge wamesema taarifa hizo za msiba huo
wamezipokea kwa masikitiko
makubwa kwa kuwa mpaka jana jioni
kabla ya kifo chake walikuwa naye
Bungeni lakini leo hawapo naye tena.
Awali kabla taarifa za
msiba huo waziri wa afya na ustawi wa jamii
akiwasilisha Bajeti ya wizara yake amesema sekta
ya afya inakabiliwa na changamoto ya
upungufu wa wawatumishi kwa asilimia 58
.
Nao watu wa sekta ya afya wamesema
serikali bado haijaweka msisitizo mkubwa
katika utafiti wa dawa mbalimbali ili
kukabiliana na tatizo la upungufu wa dawa kwani
baadhi ya dawa zilizopo sasa hivi
zingine zinaonekana kushindwa kufanya kazi na
hivyo kunatakiwa dawa mbadala.
0 comments:
Post a Comment