Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu Bwana FREDERICK SUMAYE
amesema akiteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya urais na kupewa ridhaa
hiyo, kipaumbele cha serikali yake ni kuimarisha uchumi.
Akitangaza nia ya kugombea urais
katika uchaguzi mkuu ujao, Bwana SUMAYE ameyataja mambo mengine atakayoyapa
kipaumbele kuwa ni kuimarisha elimu,kilimo,kulinda viwanda kwa kuboresha kilimo
pamoja na kupambana na rushwa na ufisadi na kusisitiza kuwa ataunda mahakama
maalum ya kushughulikia kesi za rushwa ufisadi na uhujuju uchumi.
Amesema uchumi wa nchi ukiimarika
utawezesha mengine kuimarika ikiwemo elimu, kilimo, afya na kupunguza tofauti
kati ya walio nacho na wasio nacho.
Pia
amesema kuwa kupenda na kuwa kumbatia wala rushwa bila maamuzi mazito
niswala ambalo halikubaliki na yeye hawandi na anawachukia kwa nguvu
zote,kwani kumkumbatia mlarushwa nisawa na kuchanganya Maji na mafuta
jambo ambalo ni vitu viwili tofauti.
Kuhusu
suala la maslahi ya taifa si la mchezo mchezo kama wanaojinadi kuwa
watamaliza matatizo mbali mbali ikiwemo rushwa yenye harufu kali,swali
analojiuliza wakati wapo ndani ya uongozi wameshindwaje kumaliza
tukiwapa muongo wakuongoza taifa wataweza?amesema hilo sijambo jepesi na
atashangaa kama chama kitateua mtu yeyote mwenye harufu ya rushwa
kuongoza taifa yeye atang'atuka na atalipinga vikali kwakuwa haiwezekani
mla rushwa aongoze taifa.
Mheshimiwa Sumaye anasema hivi,Nimekumbana na mambo magumu katika miaka hio kumi ikiwemo ajali ya MV Bukoba na ajali ya treni, ukame wa mwaka 1997. Niliunda kamati ya kushughulikia jambo hilo na kuchimba visima zaidi ya 300 Dar es Salaam. Mambo magumu yalinikomaza katika uongozi. Mvua za El nino zilifata baada ya ukame, ilikuwa hali ya hatari lakini tulijikwamua na tuliendelea na kazi wa kujenga taifa letu. Kifo cha baba wa taifa, mimi sikulala siku tatu nzima hata kwa nusu saa, sijawahi kuona kipindi cha amani kama kili, polisi waliripoti hata uhalifu haukuwepo.
Wakati waziri mkuu, sikuweza kusikia watu wanapigana, asubuhi nisiwepo pale, leo wakulima na wafugaji wanapigana miezi sita sasa. Mfano mgogoro wa waancholi na wahadzabe.
Huwezi kuzungumzia amani wakati watu wana njaa, tatizo la uchumi, watu wanaangalia takwimu badala ya uhalisia. Tunatakiwa tuendeleze kilimo, hata wakati wa Nyerere tulileta matrekta lakini tuliendelea? Kuleta matrekta ni jambo jema sasa nitalima heka 50, lakini uwezo wa mbegu heka 3 na kupalilia heka 3.
Eneo lingine muhimu ni masoko, lazima kiendelezwe katika ukubwa wake. Wakulima watauza kwa bei ya hasara na bei ikiwa vizuri hawana tena mazao. Leo viwanda vya sukari, hatuwezi kuingiza sukari kutoka nje bila kodi, lazima tulinde viwanda vyetu vya ndani. Mazao yetu yote, kama tutakua na juhudi za kusindika mazao, hili tatizo la ajira ambalo tunapiga nalo kelele sana, litapungua. Pia pengo kati ya walionacho na wasio nacho litapungua.
Nimeona shule binafsi wanafanya vizuri, wanataka wazipunguze nguvu, ongeza juhudi nawe umfikie. Katika miaka miwili au mitatu tutapunguza kwa kiasi kikubwa wanaoenda nje.
Rushwa na ufisadi, hili jambo sina utani nalo. Ukituhumiwa kwa rushwa ndani ya wiki moja unachunguzwa na wiki mbili mahakama imekuhukumu na kama ni viboko unapokea kabisa. Kaulimbiu yake ya uongozi ni Komesha Rushwa, Imarisha Uchumi.
0 comments:
Post a Comment