Image
Image

Mkutano kuhusu watu wenye ulemavu kuangazia Ukoma.


Kujumuisha haki za watu wenye ulemavu katika ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 ni hoja kuu kwenye mkutano wa Nane wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu unaoanza leo jijini New York ukilenga kuhakikisha haki za wakazi bilioni Moja wa dunia hii wanaoishi na ulemavu.
Kwa mara ya kwanza kabisa mkutano huo wa siku tatu pamoja na mambo mengine utakuwa na mjadala kuhusu ukoma kwa kuzingatia ugonjwa huo unaotibika bado unasalia kusababisha ulemavu miongoni mwa wagonjwa.
Sanjari na kupata changamoto wanaposaka matibabu dhidi ya Ukoma, wagonjwa wanakumbwa pia na unyanyapaa na ubaguzi kwenye jamii zao. Masuala mengine yatakayopatiwa kipaumbele anafafanua zaidi Catalina Devandas-Aguilar, mtaalamu maalum wa haki za watu wenye ulemavu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment