Kamishna Zeid ametoa wito kwa mamlaka za
Burundi kuchukua hatua za dhati kuwadhibiti wanamgambo hao na vitendo vyao.
Amesema kila siku, Ofisi ya Haki za binadamu
hupokea simu 40 hadi 50 kutoka kwa watu wenye hofu kubwa kote nchini, wakiomba
ulinzi au kuripoti dhuluma. Rupert Colville ni msemaji wa Ofisi ya haki za
bindamau, Geneva
“Tumepokea pia maelezo kutoka kwa wakimbizi waliokimbilia nchi jirani kuhusu ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaoripotiwa kufanywa na wanamgambo wanaounga mkono serikali, wakijulikana kama Imbonerakure. Uhalifu huo unadaiwa kufanyika Bujumbura na katika mikoa mingine, ukiwemo mauaji, utekaji nyara, utesaji, vipigo na vitisho vya kifo na aina nyingine za unyanyasaji.”
Bwana Colville amesema taarifa hizo ni kutoka
kwa wakimbizi 47 waliohojiwa na maafisa wa haki za bindamu katika kambi za
wakimbizi nchini Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
0 comments:
Post a Comment