Ikiwa tayari jitihada za serikali ya Tanzania
na wadau wa afya zimewezesha kudhibiti mlipuko wa Kipindupindu miongoni mwa
wakimbizi wa Burundi na wananchi huko Kigoma nchini humo, mmoja wa wataalamu wa
afya walioshiriki jitihada hizo ametaja kile kilichofanikisha udhibiti wa
haraka wa ugonjwa huo.
Jacob Lusekelo ambaye ni mwanasayansi wa
maabara kutoka Maabara kuu ya Taifa nchini humo ameiambia Idhaa hii kuwa hatua
ya shirika la afya ulimwenguni, WHO kusaidia kuongeza nguvu ya watendaji ni
moja ya siri.
Alisema "hiyo ilikuwa ni fundisho na sasa hatua zimechukuliwa kudhibiti iwapo mlipuko unatokea tena
Ugonjwa wa Kipindupindu ulilipuka mkoani
Kigoma na kusababisha vifo vya watu 30 baada ya mmiminiko wa wakimbizi kutoka
Burundi kuingia nchini Tanzania kufuatia ghasia nchini mwao.
0 comments:
Post a Comment