Mhe. Jamse Lembeli
ametoa kauli katika mkutano wa hadhara wilayani kahama kufuatia malamiko ya
wananchi waliwakilisha katika mkutano na kudai kuwa kumekuwepo na baadhi ya
viongizi wa CCM wanapita na wagombea na kuwalazimisha wananchi wawapigie kura
na kugawa kadi feki kwa watu wasiyo wanachama ili kuwang’oa viongozi wapinga
ufisadi.
Ndipo ukifika
wakati kwa Mhe. James Lembeli kusema wilaya ya kahama imetapakaa kadi feki za CCM
na kutoa angalizo kwa viongozi wa CCM kuwa wasipo badilika watavuna
mabuwa kwani watanzania wa sasa siyo wa wakati uliyopita hivyo CCM inapaswa
kuwa makini kwani hata hivyo viongozi hawo wamekiuka tamko la makamu mwenyekiti
wa CCM taifa mzee PHILIPO MANGULA alilolitoa mkoani dodoma.
Katika mkutano
huo pia wananchi walipata nafasi ya kueleza kero zao zikiwemo za watendaji
kulazimisha wawekezaji kuweka katika maeneo ambayo wananchi hawakuridhia
kuyatoa na baadhi ya wanawake kulalamikia huduma mbovu za afya na rushwa
kwa wajawazito na watoto katika hospitali na vituo vya afya.
Sorce ITV.
0 comments:
Post a Comment