Image
Image

Mabadiliko ya maendeleo na uchumi katika mikoa Ya na Lindi yatatokana na wakazi wake.


Wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi  wameelezwa  kuwa ,mabadiliko ya maendeleo na uchumi katika mikoa hiyo yatatokana na wakazi wake kuanza kuleta mabadiliko hayo na Serikali kuwa sehemu ya kuchagiza maendeleo hayo na si vinginevyo.
Kauli hiyo  imetolewa na  Mkuu wa Mkoa wa Lindi  Hajat  M WANTUMU MAHIZA  alipokuwa  akifunga kongamano la siku moja ,lililokuwa likijadili ukusanyaji maoni rasimu ya mkakati wa mawasiliano sekta ya mafuta na gesi,lililofanyika  Mkoani Mtwara amba lo li liandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini.
Amesema inaweza kuonekana ni jambo gumu kidogo ,lakini haku na namna mchango wa kwanza wa maendeleo ni lazima utokane na wananchi wa mikoa hiyo, lak ini pia wawe tayari kuondoa dhana ya Serikali ndiyo yenye wajibu wa kuwaletea mabadiliko hayo.
Ametaka watambue kuwa wakati ni huu wa kuandaa mabadiliko katika fikra zao ili wazione fursa na kuzitumia katika uchumi mpana wa gesi katika kujiletea maendeleo kupitia  nyanja mbalimbali ikiwemo ya uchumi na  jamii.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment