Wanafunzi 270 wa Chuo cha Ualimu Korogwe ,waliochaguliwa na
Serikali kusomea Stashahada ya Juu ya Sayansi na Hisabati kwa lengo la
kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo nchini,wanakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo ukosefu wa maji
chuoni hapo hatua waliyoielezea kuwa inaweza kusababisha magonjwa ya milipuko.
Wakizungumza chuoni hapo wakati viongozi wa Serikali wa wilaya na mkoa wa Tanga walipotembelea na kukabidhiwa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na
Hifadhi z a Taifa - TANAPA - kupitia Hifadhi ya Mkomazi kwa
lengo la kuwapunguzia matatizo wanafunzi hao,wamesema mbali na ukosefu wa
maji pia wameathirika kiuchumi hivyo wameikumbusha Serikali kutekeleza ahadi
yake ya kuwapatia mikopo ili
wajinunulie vifaa v itakayowawezesha
kusoma kwa ufanisi .
Kuhusu mikopo msemaji wa wanafunzi hao,LOTAMWANG'AKI MOLLEL
amesema kuna ahadi iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara y a Elimu na Mafunzo ya Ufundi ,Profesa
SIFUNI MCHOME kuwa wa tawezeshwa mikopo ili wafikie malengo yao kwa ufanisi.
Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa chuo hicho ,Bwana JAM ES MMBAJI amesema chuo kina kisima cha
maji ambayo yanatoka muda wote ,lakini hayatoshelezi mahitaji.
0 comments:
Post a Comment