KLABU
ya soka ya Mtibwa Sugar ya Turiani Morogoro imeamua kuachana na kocha
Mbelgiji Piet De Mol iliyokuwa iingie naye mkataba wa kuifundisha msimu
wa mwaka 2015/2016.Akizungumza
na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser alisema
kocha De Mol alifika nchini kwa mazungumzo ambapo walizungumza naye,
lakini wameshindwa kuingia naye mkataba kutokana na sababu zilizo nje ya
uwezo wao.
“Ni
kweli kocha huyo alikuja mpaka Manungu, akakagua kambi, lakini kwa
bahati mbaya sana tumeshindwa kusainiana naye mktaba kutokana na sababu
zilizo nje ya uwezo wetu,” alisema Bayser.
Alisema hivyo timu itaendelea kuwa chini ya kocha Mecky Maxime ambaye anaendelea na usajili kwa ajili ya msimu mpya.
“Kwa
hiyo mpaka sasa timu itaendelea kuwa chini ya Mecky mpaka hapo
itakapotangazwa vinginevyo, na tayari ameanza kufanya usajili, si kwamba
hatufanyi usajili kama wengine wanavyosema tunafanya chini ya kocha
wetu Mecky na tunaamini tutakuwa na timu nzuri msimu ujao,” alisema.
Mtibwa
Sugar iliyowahi kufanya vizuri miaka ya nyuma na kutwaa ubingwa msimu
wa mwaka 1999 na 2000, imekuwa ikiporomoka siku hadi siku ikiwa
haijarudia makali yake kwa zaidi ya misimu mitano.
Licha
ya kuanza vizuri msimu uliopita na kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa
muda mrefu, lakini ilijikuta ikivurunda kwenye mzunguko wa pili na
kufikia hatua ya kupambana kutoshuka daraja. Ilimaliza ligi ikiwa nafasi
ya saba baada ya kufikisha pointi 31 sawa na JKT Ruvu, Ndanda na Stand
United.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment