Tamasha hilo litafanyika Juni 13 kwenye
Uwanja wa Taifa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal amealikwa kuwa mgeni
rasmi.
Mzee Jangala mesema ana haki na sifa zote za
kugombea nafasi hiyo ya juu, kama waliotangulia kutangaza nia na kuwataka
wananchi kutombeza kwa uamuzi wake.
Mzee Jangala, ambaye mara nyingi huigiza kama
mzee mbishi na mwenye kauli za vichekesho, amesema Watanzania hawana budi
kusubiri kusikia sera zake na mikakati yake endapo akifanikiwa kupata nafasi
hiyo.
“Nimepanga kutangaza nia ya kugombea urais
siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib
Bilal, ambaye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la kihistoria la ngoma za
asili,” alisema Mzee Jangala.
“Najua watu watafikiria natania katika jambo
hili. Lakini siko hivyo. Nina uhakika na ninachokisema kwani ni haki ya kila
raia na inatambulika kikatiba kugombea nafasi hii nyeti endapo tu ukiwa unazo
sifa na vigezo,” alisema Mzee Jangala.
Msanii huyo mkongwe, ambaye hakutaja
atagombea kwa chama gani, alisema kilichomsukuma kutangaza nia kwanza ni
mzalendo na mapenzi kwa nchi yake.
“Pili ni kuondoa tatizo la mmomonyoko wa
maadili kwa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana na wananchi,” alisema msanii
huyo aliyeanzia katika uigizaji wa jukwaani.
Alisema baadhi ya viongozi wakipewa madaraka
wanasahau walikotoka na kutenda mambo kinyume na matarajio ya wananchi. Hali
inayosababisha shughuli wanazozifanya kutofanyika ipasavyo na kuibua
minung’uniko.
“Hawa tuliowachagua, baadhi yao hawana
uchungu na nchi hii ndiyo maana rushwa imekuwa sehemu ya maisha yetu, kwa
sababu walioko madarakani wapo kwa masilahi yao binafsi na si ya Watanzania,”
alisema Mzee Jangala.
“Rushwa imekuwa changamoto mojawapo, sasa
basi mimi nina uwezo, najiamini kuongoza na kupambana na jambo hili.
Kinachohitajika kwa Watanzania kuniunga mkono pindi nitakapotangaza nia yangu.”
Hata hivyo, Mzee Jangala hakuwa tayari kutaja
vipaumbele vyake endapo atapata nafasi ya kugombea urais akisema kuwa bado ni
mapema sana. Ukizingatia kuna wimbi kubwa la Watanzania wanaotarajia kutangaza
nia ya nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment