Jumla ya msafara wa watu 34 uliondoka jana
kuelekea Addis Ababa, nchini Ethiopia, kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na
mchezo huo, wakiwemo wachezaji 23, benchi la ufundi lenye watu saba na viongozi
wanne wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Nooij
aliahidi mambo matatu, kuonyesha kandanda safi, ushindi, kufanya mambo tofauti
na ilivyokuwa kwenye michuano iliyopita ya COSAFA, ili kuweza kurudi kamili
kujiandaa na michuano ya CHAN dhidi ya Uganda, mchezo utakaochezwa Zanzibar.
“Tutaitumia vizuri kambi hiyo ya wiki moja
kabla ya kucheza na Misri, nina imani tutaibuka na ushindi na Watanzania
wategemee hilo na tuna uhakika huo,” alisema.
Wachezaji wanaosafiri kuelekea nchini
Ethiopia ni Makipa Deogratias Munish ‘Dida’, Aishi Manula na Mwadini Ali.
Walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto
Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma Abdul.
Viungo Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum
Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla.
Washambuliaji Saimon Msuva, John Bocco,
Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Mrisho Ngasa na Juma Liuzio.
Wakati hao wakielekea Ethiopia, wachezaji
waliobaki wanatarajia kuondoka nchini kesho, kuelekea nchini Rwanda kucheza
mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Rwanda katika kumbukumbu ya mauaji ya
kimbari.
Wachezaji hao ni Peter Manyika, Said Mohamed,
Emmanuel Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan Isihaka, Gadiel Michael na Hassan
Dilunga.
Wengine ni Rashid Mandawa, Atupele Green,
Kelvin Friday, Hassan Kessy, Ibrahim Ajib, Malimi Busungu, Mudathir Yahya, Deus
Kaseke, Andre Vicent, Amri Kiemba na Mohamed Hussein.
0 comments:
Post a Comment