Kwenye ajenda ya mkutano wa
marais kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo Jumapili, masuala kadhaa
yatazungumziwa kama mzozo wa kisiasa Burundi, kuongezeka kwa makundu ya kigaidi
barani Afrika au mgogoro wa Sudan Kusini.
Lakini pia litazungumziwa
katika mkutano huo suala tata la vijana wengi kutoka barani wanaoelekea Ulaya
wakipitia katika bahari ya ambapo wamekua vijana wengi wamepoteza maisha
kutokana na kuzama kwa boti wanazotomia katika safari hizo za majini.
Mkutano huo wa viongozi wa
nchi kutoka bara la Afrika unaoanza kesho jumapili pia utajadili juu ya mgogoro
unaolikumba taifa la Sudan Kusini lakini pia mikakati ya pamoja katika
kuimarisha pambano dhidi ya ugaidi barani Afrika.
Msemaji wa Rais Pierre Nkurunziza
wa Burundi hata hivyo amesema kiongozi huyo hatahudhuria mkutano huo.
Leo Jumamosi na Jumapili,
suala litakalojadiliwa kwa upana ni namna ya kutuliza machafuko yanayoendelea
nchini Burundi kutokana na hatua ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwa atawania
urais kwa muhula wa wa tatu.
0 comments:
Post a Comment