ALIYEKUWA
mchezaji hatari wa timu ya Yanga msimu uliomalizika,Mrisho Ngassa
amefanya mazoezi na timu yake hiyo ili kujiweka sawa kabla ya kuelekea
nchini Afrika ya Kusini.
Ngasa amesajiliwa na timu ya Free State ya Afrika Kusini baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga msimu wa ligi wa 2014/15.
Mchezaji
huyo ambaye alionesha kiwango kizuri aliisaidia kwa kiasi kikubwa timu
yake hiyo ya zamani kuchukua ubingwa mapema kwa kufikisha pointi ambazo
sizingefikiwa na timu nyingine katika ligi kuu iliyomalizika.
Akizungumza
baada ya mazoezi hayo yanayofanyika katika uwanja wa Karume jana, Ngasa
alisema kuwa ameamua kufanya mazoezi na timu yake ya zamani ili
kujiweka sawa.
Alisema, anahitaji kujiweka sawa kwa ajili ya ligi kuu ya nchini Afrika ya Kusini ambayo itaanza hivi karibuni.
Alisema kuwa kwa sasa anachokisubiri ni ripoti ya uongozi wa klabu yake hiyo ili kujua inaingia kambini lini.
"Kwa
sasa nipo nyumbani nikisubiri ripoti ya uongozi kujua timu inaingia
lini kambini ili niweze kujiunga na wenzangu kambini," alisema Ngassa.
Mchezaji huyo mwenye kasi ya ajabu amesema atahakikisha anaendeleza makali yake katika timu yake hiyo mpya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment