Mfalme wa muziki wa Taarab nchini mzee Yusuph Atangaza nia kugombea ubunge.
MKURUGENZI wa Bendi ya Muziki wa Taarab ya Jahazi, Mzee Yusuph, ametangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Fuoni, Unguja kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Mzee ambaye pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya timu ya Yanga, alisema ni wakati wa kutimiza ndoto zake za siku nyingi na kuingia katika kinyang’anyilo cha kuwania nafasi hiyo.
Alisema licha ya kujaaliwa kipaji cha muziki, lakini kwa miaka mingi amedhamiria kuwa mwanasiasa, na sasa anaanza safari hiyo kwa kuomba ateuliwe kuwania kiti cha ubunge.
Alisema anajua siasa ngumu, lakini amejipanga kuhakikisha anapata nafasi ya kuwania kiti hicho ili aweze kuwawakilisha wananchi wa Fuoni.
“Najua siasa ni ngumu, lakini kwa kuwa najitambua nitahakikisha ninapata nafasi hiyo,”alisema Mzee.
Jimbo hilo kwa sasa, linaongozwa na Mbunge, Said Mussa Zuberi.
0 comments:
Post a Comment