Image
Image

Profesa Ndulu atetea noti za Tanzania


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu amesema karatasi zilizotumika kutengeneza noti za Tanzania zina ubora kwa kuwa wataalamu wamezithibitisha. Ndullu alizungumza hayo jana mjini Dodoma wakati wa semina ya wabunge iliyojadili kuporomoka kwa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa.
Katika siku za karibuni kumekuwapo na manung’uniko mbalimbali kuhusu ubora wa noti za Tanzania kuwa hazina ubora na zinachakaa haraka hasa noti ya Sh500.
Profesa Ndulu alisema kuwa noti ya Tanzania haikutengenezwa tu, imeangaliwa na wataalamu na mazingira yake kuwa ni joto na katarasi yake imetengenezwa kwa pamba.
Akifananisha na noti ya Malaysia pamoja na Singapore, Canada na nchi nyingine kuwa zimetengenezwa kwa nailoni kwa kuwa ni nchi za baridi. Noti za Tanzania ziko za aina tano, Sh500, Sh1,000, Sh2,000, Sh5,000 na Sh10,000.
Akizungumzia kuporomoka kwa shilingi alisema, Benki Kuu imeanza kudhibiti biashara ya fedha za kigeni, mikopo ya fedha hizo kwa benki za ndani na nje na kupitisha kanuni za kushiriki katika soko la fedha za kigeni.
Wabunge mbalimbali walichangia hoja hiyo akiwamo, Idd Azzan aliyetaka BoT kuyabana maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kwa kuwa yanatumika kutakatisha fedha chafu huku Ole Medeye aliitaka BoT kutoa maelezo kuhusu fedha za PAP. Profesa Ndullu aliwataka wabunge kuingia katika masoko ya hisa na kusema wamepokea hoja hizo za wabunge.na watazifanyia kazi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment