Image
Image

Rais Jacob Zuma awakingia kifua askari waliowaua wafanyakazi 34 katika mgodi wa Marikana.


Rais JACOB ZUMA wa Afrika ya Kusini ametetea polisi waliowaua kwa kuwapiga risasi wafanyakazi 34 waliokuwa kwenye mgomo katika mgodi wa Marikana wa Kampuni ya Lonmin mwaka 2012.
Akizungumza siku chache kabla ya kuchapishwa ripoti ya matokeo ya uchunguzi wa tukio hilo baya zaidi la maafa kuwahi kufanywa na majeshi ya usalama tangu kumalizika ubaguzi wa makaburu Bwana ZUMA alisema watu wa Marikana walikuwa wameuana polisi walikuwa wanazuia wasiue watu zaidi.
Alikuwa akijibu swali alililoulizwa wakati wa ziara yake kwenye chuo kikuu kimoja cha Pretoria baada ya taarifa kwamba Bwana ZUMA alikuwa tayari amepokea matokeo ya uchunguzi wa mauaji hayo ya Marakane miaka mitatu iliyopita.
Mbali na mauaji ya kwenye mgodi huo watu wengine kumi pia waliuawa katika machafuko ya mgomo huo wa wachimba migodi wakiwemo polisi wawili waliokatwa vichwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment