Image
Image

Marekani ilifanya ujasusi kwa marais wa Ufaransa.


Marekani ilifanya ujasusi kwa marais wa Ufaransa ambapo mtandao wa WikiLeaks  unasema Shirika lake  la Usalama wa Taifa lilidukua mawasiliano ya Rais FRANCOIS HOLL ANDE na watangulizi wake wawili  NICOLAS SARKOZY na JACQUES CHIRAC.
Vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema kuwa udokozi huo ulifa nywa katika ya miaka ya 2006 na  mwaka 2012 na tovuti ya watoa taarifa za siri imeonyesha taarifa na nyaraka za siri za kiufundi kutoka Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani.
Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani imesema kwa kawaida huwa haizungumzii nyaraka  zinazofichuliwa au kuvujishwa na mtandao huo wa Wiki - Leaks.
Msaidizi wa Rais HOLLANDE amesema alikuwa ameitisha leo mkutano wa baraza la ulinzi kujadili suala hilo ambapo imefahamika mwaka 2013 Shirika hilo la Ujasusi la Marekani pia lilituhumiwa kwa kumfanyia ujasusi Kiongozi wa Ujerumani Bibi ANGELA MERKEL.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment