Shirika la Afya Dunia (WHO) limetahadharusha kuwa kesi za maambukizi ya homa ya dengue zimeongezeka nchini Yemen tangu Saudi Arabia ianze kuishambulia nchi hiyo mwezi Machi mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na WHO imesema kesi 3000 zinazodhaniwa kuwa za homa ya dengue zimeripotiwa nchini Yemen tangu mwezi Machi mwaka huu na kwamba idadi ya kesi hizo inatazamiwa kuwa kubwa zaidi. Msemaji wa WHO, Christian Lindmeier amesema baadhi ya mashirika yasiyo ya serikali yameripoti kuwa kesi za homa hiyo zimefikia 6000 ambazo ni mara mbili zaidi ya zile zilizoripotiwa rasmi.
Mamilioni ya Wayemeni hawana huduma za maji na afya kutokana na mashambulizi ya kinyama ya anga yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa nchi hiyo. Mashambulizi ya kijeshi ya Saudia huko Yemen yanalenga zaidi miondombinu na maeneo ya raia ikiwemo misikiti, shule na vituo vya afya.
0 comments:
Post a Comment