Mhe. Jaji Mugasha akitia sahihi hati ya kiapo mara
baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
Majaji
wapya wawili wa mahakama ya rufaa Augustine Mwarija na Stella-Esther Mugasha wamesema changamoto inayowakabili ni
ya kuhakikisha haki inatendeka na kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuondoa
msongamano wa mashauri.
Majaji
hao wameyasema hayo ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa na Rais
Jakaya Kikwete kuwa majaji wa mahakama ya rufaa wakitokea mahakama kuu ambapo Mwarija,
alikuwa jaji mfawidhi, mahakama kuu, divisheni ya biashara huku mugasha
akiwa jaji mfawidhi mahakama kuu kanda
ya Dar es Salaam.
Wakizungumza
katika hafla fupi iliyofanyika ikulu majaji hao wameahidi kutumia uzoefu
walionao katika kukabiliana na changamoto ya wingi wa mashauri katika mahakama
hiyo kwa kutumia utaratibu wa kushughulikia kwanza mashauri ya yaliyochukuwa
muda mrefu kutolewa maamuzi.
0 comments:
Post a Comment