Image
Image

Watu 18 wameuawa na wengine 98 wamejeruhiwa baada ya treni ya abiria kugongana na lori huko Tunisia.


Watu 18 wameuawa na wengine 98 wamejeruhiwa baada ya treni ya abiria kugongana na lori huko Tunisia huku kukiwa na taarifa kwamba hakukuwa na kizuizi wala ishara kwenye kivuko cha reli na barabara.

Ajali hiyo ilitokea El Fahes kiasi cha kilomita 60 kusini-magharibi ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis wakati wa asubuhi ambapo kunakuwa na heka heka nyingi za watu wanapokwenda kwenye shughuli zao.

Mashuhuda aidha walielezea jinsi mabehewa yalivyokuwa yameharibika na kutapaa kwa miili.

Maafisa wanasema watu 30 bado wamelazwa hospitalini kwa matibabu wakati wengine wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment