Image
Image

Rais Kikwete:Sina mgombea ninaye mpendelea miongoni mwa wagombea Urais.


Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE amesema  hana mgombea miongoni mwa wagombea Urais ambaye anampendelea kwa sababu wagombea wote ni wa kwake na ni wa chama chake.
Amesema anayo kura moja tu ambayo ataitumia mwezi ujao wakati wa vikao mbalimbali kuamua nani awe mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi  katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya Habari, Rais KIKWETE ameyasema hayo Mjini Johannesburg, Afrika Kusini alipokuwa akizungumza na  Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje wa Marekani, anayeongoza Kitengo cha Masuala ya Afrika Bi. LINDA THOMAS-GREENFIELD.

Pia amesema hana tatizo na kujitokeza kwa wagombea wengi wa nafasi ya Urais zamu hii kupitia Chama cha Mapinduzi  kwa sababu huwezi kuwazuia watu kugombea nafasi hiyo kwa sababu ni haki yao.

Viongozi hao wawili walikuwa wanahudhuria Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Sandton Mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment