Serikali
imesema itaendelea kuboresha miumbombinu ya Tehama katika shule mbalimbali
nchini ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kusoma na kupata
taarifa mbalimbali zitakazo wasaidia katika masomo yao kwa nyia ya Tehama.
Kauli
hiyo ya serikali imetolewa jijini Dar es Salaam na katibu mkuu wa wizara ya
mawasiliano,sayansi na tekinolojia Proffesa .Patrick Makungu muda mfupi baada
ya kuzindua mpango wa matumizi ya Compyuta katika shule za wanafunzi wenye
mahitaji maalum na mchanganyiko ambapo amesisitiza ni lengo la serikali kuona
kila mwanafunzi ananufaika na mfumo wa Tehama.
Kwa
upande wake afisa mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa umma Enginea Peter
ulanga amesema ni lengo la taasisi yake kuhakikisha inafikia shule zaidi ya
shule 200 za wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha waendane na
changamoto za ukuwaji wa tekinolojia.
Jumla
ya shule 4 za watoto wenye mahitaji maalum zimenufaika na mradi huo ambapo kompyuta
zaidi ya 35 zimetolewa kwa shule hizo huku mwalimu mkuu wa shule ya uhuru
mchangayiko akielezea jinsi walivyo nufaika na mradi huo.
0 comments:
Post a Comment