Serikali
imesema inaendelea na kampeni ya nyota ya
kijani kwa nchi nzima ili kuelimisha jamii juu ya mpango wa uzazi kwa lengo
la kulinda afya ya wanawake na watoto na
kudhibiti ongezeko la watu kiholela.
Akijibu
swali Bungeni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. KEBWE STEPHEN KEBWE
amesema pamoja na kampeni hizo za uhamasishaji wa nyota ya kijani mbinu
mbalimbali pia zimekuwa zikitumika kuhamasisha jamii zikiwemo kutumia redio na
televisheni, vipeperushi na mabango.
Naye
Naibu Waziri wa Uchukuzi DR. CHAROES TIZEBA ameliambia Bunge kwamba Serikali
kupitia Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania-TPA- imeanza kulipa fidia kwa
wakazi wa eneo la BUTUNGU na KATOSHO katika manispaa ya Kigoma Ujiji ili
kupisha mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu katika eneo hilo.
Akijibu
swali amesema tathimini imebaini kuwa zaidi ya shilingi bilioni 12 zinahitajika
kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wakazi elfu moja na mia mbili na 28
watakaopisha eneo hilo la mradi.
Wakati
huo huoSerikali imepanga kutaifisha mali za watuhumiwa waliohusika kuwaingiza
raia wenye asili ya India na Nepal nchni kwa ajili ya kufanya kazi zisizokuwa
za heshima katika klub za usiku jijini dare s salaam.
Akijibu
swali Bungeni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani PERREIRA SILIMA Amesema raia hao
walipata vibali sahihi kutoka idara ya uhamiaji na baraza la Sanaa Tanzania kwa
misingi ya kufanya kazi halali za usanii wa ngoma zenye asili ya utamaduni wa
India na Nepali lakini walikiuka masharti
ya vibali hivyo na kurejeshwa makwao.
0 comments:
Post a Comment