Image
Image

Serikali na Benki ya Afrika wakubaliana kujenga kwa kiwango cha lami barabara kutoka Mpanda hadi Pangale Tabora.


Serikali iko katika hatua za mwisho kukamilisha mazungumzo na Benki ya Maendeleo  ya Afrika  ambapo wamekubaliana kutoa fedha za mkopo kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara  kutoka Mpanda hadi Pangale Tabora yenye umbali wa Kilo mita 334.

Kauli  hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi ,GERSON LWENGE  alipokuwa  akijibu swali  la mbunge wa Mpanda Mjini SAID ARFI aliyeuliza ni lini serikali itajenga barabara ya lami ya kuunganisha wilaya Mpanda,Mlela,Sikonge na Tabora.

Naibu Waziri a mesema serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara yote kutoka Mpanda hadi Tabora.

Amesema serikali ya Tanzania kwa kutumia fedha zake za ndani imeanza kujenga sehemu ya Pangale hadi Tabora yenye urefu wa kilomita 30 chini ya wakala wa barabara nchni TANROADS.

Bunge limeelezwa kuwa  Serikali imeunda kamati za mikoa na kitaifa kushughulikia   matatizo ya  utumaji wa mashine za kutolea  stakabadhi   za -EFD- kwa kushirikisha viongozi wa Serikali za mikoa na wadau wengine katika  kuhimiza  matumizi ya mashine hizo.

Naibu Waziri wa Fedha ADAM MALIMA amesema lengo la kamati hizo ni kutatua migogoro na malalamiko yanayotokana na usimamizi wa matumizi ya EFD kwa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa matumizi ya EFD na kupendekeza hatua za kuchukua ili kuboresha ufanisi wa mfumo huo ikiwa ni pamoja na kupanua elimu kwa umma.

Kauli hiyo ya serikali imekuja kufuatia swali la mbunge wa viti maalum  AMINA AMOUR aliyeuliza serikali ina mkakati gani wa makusudi wa kuhakikisha mashine hizo zinafanya kazi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment