Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti wa NEC,
Jaji Damian Lubuva alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
“Sheria haijabadilishwa ili kuruhusu vituo vya kupigia kura katika magereza na monitoring (uangalizi).
Pia
kunatakiwa kuwe na vibali kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani,” alisema Jaji
Lubuva.
Alisema bado hawajakutana na Serikali
kujadili suala hilo.
“Tukishakaa pamoja sasa tutakuwa na cha kuwaambia wananchi,” alisema.
Hivi karibuni Kamati Kuu ya CCM iliishauri
serikali kukaa na Nec na kutafuta njia muafaka ya kulishughulikia kwa
kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumzia changamoto, Jaji Lubuva alisema
suala la watu kuchukua muda mrefu katika uandikishaji hutokea wakati mashine
zinapokuwa na tatizo.
“Mtu mmoja anachukua dakika mbili hadi nne kuandikishwa, labda panapotokea tatizo katika mashine ama uchukuaji wa alama za vidole lakini maofisa waandikishaji hulitatua kwa kipindi kifupi,” alisema.
Kuhusu baadhi ya watu kuachwa bila
kuandikishwa, Jaji Lubuva alisema hakuna mtu aliyeachwa kituoni bila
kuandikishwa.
“Kilichojitokeza baadhi ya viongozi wa kisiasa huenda kwa wananchi na kuwauliza nani aliyeachwa bila kuandikishwa, lakini si kwamba waliokwenda vituoni hawakuandishwa,” alisema.
Jaji Lubuva alisema malalamiko yaliyotolewa
na katibu mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa kuhusu haki ya wanafunzi wa vyuo
vikuu kuandikishwa, siyo ya kweli.
Alisema wanafunzi hao pamoja na wananchi
wengine wanayo nafasi ya kubadilisha taarifa zao muda wowote.
0 comments:
Post a Comment