Amesema kama kitambulisho hicho
kingeboreshwa kingeweza kutumika kwa ajili ya kupiga kura, hivyo kusingekuwapo
uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Waziri huyo aliyasema hayo
jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa kongamano la kimataifa la
uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa lijulikanalo kama ‘Govetnment Forum on
Electronic Identity in Africa', unaofanyika Afrika kwa mara ya kwanza na
kujumuisha wataalam zaidi ya 300 wa ndani na nje ya Afrika.
“Kama tungejipanga mwanzo vizuri ni wazi kusingekuwapo haja ya mchakato unaoendelea wa kuandikisha kwa kutumia BVR, ni nafasi kwetu kujifunza na kujirekebisha na pia watajifunza kutoka Tanzania,” alisema.
Silima alisema siku zijazo
vitambulisho hivyo vitaboresha zaidi ili kutumika kwenye maeneo mbalimbali, na
kwamba kwa siku za usoni vitatumika kwenye malipo mbalimbali.
Aliwataka Watanzania wanaoshiriki
katika kongamano hilo kupokea na kutumia teknolojia inayotoka kwenye makampuni
mbalimbali duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu, alisema watu milioni 6.1
wameandikishwa katika maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara,
Morogoro na Tanga na kwamba watu milioni 2.5 wamepatiwa vitambulisho.
Alisema kongamano hilo
linalojulikana ‘Govetnment Forum on Electronic Identity in Africa’, limeleta
pamoja nchi 24 ambazo zitajadili kwa kina changamoto zilizopo kwenye
uandikishaji, uandaaji wa vitambulisho vya Taifa na jinsi gani vitatumika kwa
maendeleo ya Taifa.
0 comments:
Post a Comment